Pigia shoga wa mzangila simu.

= 1271

Ni wikendi hapa kwa Mzangila.com.Kama kawaida,kina dada wameenda shughuli za hapa na kule.Kina dada wa Mzangila(Robertina,dada Mary,Charity na wenu wa ubani hapa) tumestarehe kwenye visehemu vya kupokea simu.Visehemu hivi vimegawanywa na vioo na tukiwa ndani Mzangila hatuoni ngo!
Mzangila yumo afisini mwake,bila shaka anakaguakagua mafaili huku akinywa whisky yake(anapenda anasa sana kaka huyu).Falsafa yake ya maisha ni “uzuri wa pesa ni nini kama hazitumiki?”.
Kwa sababu hatuna simu za wosia wa dharura,tunajipodoa huku kwenye sehemu zetu za kazi.Mara dada Robertina anachukua kioo,mara anazifunga nywele za Charity na mimi huyo napiga hadithi moja baada ya nyingine.Kama ada tunabana kicheko au tunacheka kwa sauti ya chini sana ili Mzangila asije akasikia na kutufurusha.Katika hali hii,simu yangu inapigwa.Bila shaka ni msomaji mmoja anataka wosia.
Nampa dada Mary kioo na kurudi kwenye nafasi yangu ya kazi na kuzungumza kwenye simu hiyo.
“Karibu. Hapa ni Mzangila.com,shoga Agnes kwenye simu nani mwenzangu?”Nasema huku nikiweka kidole changu cha shahada kwenye kinywa kuwaashiria kina shoga Robertina wanyamaze.
“Mie ni Grace” Dada Yule akajibu.
“Grace?”
“Naam”
“Tukusaidie vipi dada?”Nikamuuliza
“Nilikuwa na tatizo”Akanijibu
“Kwa hivyo sasa huna?”
“Sikumaanisha hivyo”
“Hukumaanisha hivyo?”
“Mmmmh”Akajibu
“Mmmmmh”Nikamjibu pia.
“Mchumba wangu anapenda wanawake takribani wote.Hata sijui nifanye nini”Dada huyo alishtaki hali yake ya kihusiano.
“Anapenda wanawake wote?”Nilimuuliza kwa mshangao.
“Ndivyo shoga Agnes” Alinijibu.
“Vipi kupenda wana ambao ni wake liwe tatizo?” Nilimuuliza dada huyo.Kina Robertina walikondoa macho huku wakinikunjia nyuso kuwa nizungumze vizuri.
“Simaanishi hivyo” Alidakia.
“Ni hivyo ulivyoshtaki hali yako dada.Hivi kumbe wewe ni hasidi hivyo?Hutaki mchumba wako apende wanawake?Nani apende wana wake ambao yeye mwenyewe kawaza? Nilimuuliza kwa ukali huku nikiomba kopo la maji kutoka kwa dada Mary.
“Mbona unanichezea Shoga Agnes? Kaka Mzangila alisema tuwaulizeni nyie mashoga maswali.Mbona kutukejeli hivi?Nitamweleza kaka Mzangila” Grace alisema huku akiwa mwenye kukereka kwelikweli.
Kusikia hayo dada Charity alidakia simu mara moja.Alitaka kuzungumza na Grace ili asije akatushtaki kwa kumkejeli.Alikuwa amechelewa kwani Grace hakuwa kwenye simu tena.Wote waliniangalia kwa hofu.Walijua fika kuwa dada Grace akimweleza kaka Mzangila yalijojiri tutaona kilichomtoa kanga manyoya.

Use Facebook to Comment on this Post

Related Posts:

  • No Related Posts

About Agnes Sikuku

Check Also

Uchawi wa Mombasani

Post Views = 4121 Niliamka asubuhi mbichi kwa mshtuko ! Kufungua macho nikakaribiswa na magome …

SIMU YA KIFO

Post Views = 3564Ilikuwa jumamosi ya aina yake nikiwa kwenye mikiki mikiki ya wikendi. Matanuzi …

Leave a Reply

Connect with:
Your email address will not be published. Required fields are marked *