Kiswahili kitukuzwe

= 5453

Ni Ijumaa iliyo jaa mambo na vijimambo tumbi nzima. Lakini ningependa uniazime dakika chache tu nikudokezee jambo. Si msururu wa mambo. Jambo moja tu nipe lako skio.

Nasikitika kuona Kiswahili twakiua polepole. Tangu tujue kuporomosha King’eng’e basi hakitukoki mdomoni! Si shuleni si kazini hadi kwetu nyumbani tumeitukuza sana lugha ngeni.Tumesahau king’eng’e kilikuja na mbepari na chetu Kiswahili tukakizika katika kaburi la sahau. Wengine twajitia hamnazo eti Sheng’ ndio yetu lugha!

Mengi leo sitasema lakini wasia nakuachia mimi- tujifunze Kiswahili. Tukienzi kama walivyo kienzi wazee wetu. Tukikidharau sisi nani atakipenda? Ni hayo machache tu Ijumaa ya leo. Lakini sitakuacha mkono mtupu kwani mkono mtupu haulambwi,sio?

Nataka utafakari na shairi maridadi la Shaban Robert kutoka Jahadhmini ya Mashairi ya Kiswahili. Hadi tutakapo kutana tena,tukitukuze Kiswahili:

Titi la mama litamu, hata likiwa la mbwa,
Kiswahili naazimu, sifayo iliyofumbwa,
Kwa wasiokufahamu, niimbe ilivyo kubwa,
Toka kama mlizamu, funika palipozibwa,
Titi la mama litamu, jingine halishi hamu.

Use Facebook to Comment on this Post

Related Posts:

  • No Related Posts

About mzangila

Check Also

Love can do it

Post Views = 2372 Before you begin to look for my hand, let me tell …

First dates

Post Views = 7446 I do realize that that my creative mojo isn’t back yet. …

3 comments

  1. Hongera dada,tuakienzi kiswahili.Kazi nzuri.

  2. bookmarked!!, I like your web site!

Leave a Reply

Connect with:
Your email address will not be published. Required fields are marked *