Barua ya kirafiki kwa mashoga

= 6113

MASHOGA WAPENDWA,

Pokeeni salamu furifuri kama mchanga wa bahari kutoka hapa kwangu.Mie ni buheri wa afya. Hofu na mashaka ni kwenu iwapo mu wazima au mmelingwa mawe na kufariki papo hapo kama Stephano wa bibilia.

Natumai mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku,mathalani kuwafungua wenzenu “ boot” ,kuvalia long’i zilizowabana na mengine mfanyayo tusiyoyajua ambayo ni kama usiku wa giza.

Sababu ya kukuandikieni arafa hii ni kujadili na kuwapa matakwa yangu kwenu.Natumai mtayakubali.Kwanza kabisa sina ngoa nanyi.Miili ni yenu na mnaweza fanya mpendavyo.Hata hivyo vitendo vyenu vina madhara mengi.Mwajua fika madhara hayo,lakini niruhusu niyaorodheshe:

1.Kwa kuoa mume mwenzako unamkosesha mamako mzazi raha au karaha ya kumchukia mkeo,kumsuta na kucheka naye.

2.Kwa kuoa waume mabanati warembo wanakosa waume.

3.Ni hujuma ya kijamii kwa wanaume wawili wenye miraba mine kulala pamoja ilihali maskini mabinti wasio na waume wanatazama tena na tena iwapo waliubana mlango au la.

4.Mliskia wapi eti babu wa babu,babu,mjomba au baba kaoa mume mwenzake?

5.Mnapowaoa waume wenzenu na kusema ni haki yenu mnafanya neno haki lipoteze maana.Hatuwaelewi kabisa,labda mtueleze kwa michoro au cheti ili tuwapate.

6.Kuoa waume wenzenu ni kwenda kinyume na dini.Najua nimeadimika kama wali wa daku kanisani,lakini nilipokuwa huko nilielewa fika kuwa ni mapenzi ya Mungu mume amchukue mke katika maswala ya ndoa.

7.Mashoga wakiruhusiwa kuwa na familia,itakuwa vigumu kuwalea watoto wenye maadili katika jamii.

Kama nilivyosema,mwaweza kutenda mtakavyo.Hata hivyo ombi langu kwenu ni kuwa mtuone sisi mabanati.Ni jambo la kuvunja moyo iwapo sisi mabanati tunajirembua vilivyo na hamsisimki bali mwawaona waume.Mwaweza waoa na kuwa na uhusiano nao kisirisiri.Nilisikitika kusikia kuwa wenzenu waliachwa na wake zao baada ya kujulikana.Hilo lisiwatie kiwewe,tutazungumza hayo mambo.Tukigundua,kwa niaba ya wake wote naahidi kuwa hatutawafedhehesha kadamnasi ya watu.Tutaongea chemba na bila shaka tutapata suluhu.

Ni hayo tu.Natumai kusikia kutoka kwenu .

Wenu awapendaye kama dhati ya moyo wake wote.

Sahihi

Mimi

Use Facebook to Comment on this Post

Related Posts:

  • No Related Posts

About Agnes Sikuku

Check Also

Love can do it

Post Views = 1063 Before you begin to look for my hand, let me tell …

First dates

Post Views = 6371 I do realize that that my creative mojo isn’t back yet. …

2 comments

  1. Asante sana dadàngu …
    Kazi yako ni nzuri sana …kwa hakika nimeipenda…

  2. Asante paps.Endelea kusoma.

Leave a Reply to Agnes Cancel reply

Connect with:
Your email address will not be published. Required fields are marked *