SIMU YA KIFO

= 3558

Ilikuwa jumamosi ya aina yake nikiwa kwenye mikiki mikiki ya wikendi. Matanuzi ndio mpango niliokuwa nao nikiwa pamoja na mrembo wangu Amina.Pesa haikuwa gharama kwangu,ama kweli pesa dhahabu, ukiwa na pesa unaweza anzisha hata dini. Tayari nilikuwa nimekodi chumba cha malazi na kulipia orodha ya vitu ambavyo tungehitaji pale hotelini. Hoteli yenyewe iliitwa Atlantic na ilikuwa mkabala na bahari Hindi kwenye ufuo mwanana wa jiji la Mombasa.
Watu wengi hususan wapenzi walikuwa wamefurika kwenye hoteli Atlantic kujivinjari. Magari ya kifahari yalijaa pomoni kwenye maegesho ya hoteli hii kuashiria kuwa ilikuwa hoteli yenye hadhi maridhawa. Wakwasi na mabwanyenye pekee ndio waliokuwa na uwezo wa kumudu gharama za hoteli hii. Pangu pakavu na Watu hohehahe waliionea mbali.
Saa kumi na mbili ilinikuta kwenye bwawa la kuogelea. Niliogelea kwenye maji fufutende sambamba na malaika wangu Amina. Watu wote walikuwa karibu nasi walitutazama kana kwamba wameona malaika ila hakutusumbua maana tulishazoea mambo kama hayo. Siri ya watu kututazama ilikuwa urembo aliokuwa nao Amina na utanashati niliojaliwa na Maulana.
Jua lilipokiangaza kiwiliwili cha Amina, hakika hata kipofu angeweza kuona urembo wake. Nywele zake za singa, macho yake ya kiarabu, meno yake meupe pepepe, kiuno cha kupendeza, sauti yake ilikuwa ya kupendeza na yakutoa simba mawindoni. Watu waliishi kulipiga mfano penzi letu jambo lilotupa faraja na kujiona wenye bahati.
Baada ya kuogelea kwa kina nilimshika Amina mkono kimahaba kuelekea chumbani kubadilisha mavazi. Alipopita na bikini yake ya chanikiwiti ilibidi wanaume kadhaa wasutwe na wake zao kwa jinsi walivyomtazama malkia wangu kwa tamaa. Mara zote tukiwa na mahabuba, hakuacha hulka yake ya kupenda kunikumbatia kila wakati, hakika nilimpenda Amina na kumueka moyoni na kujiapia hata kwenye mtutu wa bunduki siwezi kumtoa.
Hatua iliyofuata tuliendea chajio. Meza ilijaa kaukau, nyama choma, birinzi, chipsi, mayai, biriani na vinywaji vya Tropicana.Tulilishana na mpenzi wangu huku tukizungumza kwa mahaba kana kwamba tulijuana juzi licha ya kuwa kwenye mapenzi motomoto kwa miaka miwili sasa. Njaa ilipotupaa ilikuwa muda wa saa mbili unusu nilienda kwa kaunta kulipa gharama ya malaji kisha nikaushika mkono kidosho wangu hadi kwenye chumba chetu.
Usiku ule tulifungua nyoyo zetu na kuelezana ndoto zetu za baadaye. Mawazo yetu yalifanana kama riale kwa ya pili, hakika nilibarikiwa ubavu wangu. Muda wote tukijadiliana kichwa cha Amina kilikuwa kifuani kwangu huku shungi la nywele zake likinitekenya tumboni. Niliokuwa nimeingiza vidole vyangu kwenye mianya ya vidole vyake huku miili yetu ikiwa imeumana barabara. Kila mmoja alipendezwa na mwingine.
Ilipotimu saa sita, ndipo ile hisia ya kutaka kuzima taa ilipoanza kutuingia kwenye damu. Cha ajabu hadi sasa sikuwa nimegundua kwamba mlango ulikuwa wazi, niliuregesha kwa kuukomea sikuwa nimetia ufunguo-mwanya kubana.Ghafla simu yangu iliita na nikaazimu kuichukua japo kwa woga maana sikuwa na mazoea ya kupigiwa simu usiku. Cha ajabu mpigaji hakuwa kwenye orodha ya watu niliosevu nambari zao. Ilikuwa nambari geni.
Mpigaji alinguruma kwa sauti ya kutisha kama mwanamgambo wa Al-shabab. Aliniamuru kwamba amenibebea kifo mikononi mwake hivyo amenipa dakika ishirini nitume milioni hamsini kwenye akaunti yake benki. Simu ya kifo! Nilikata simu kwa woga huku nikitetemeka kama kifaranga mwenye manyoya haba kwenye msimu wa kipupwe. Usipoajabu ya Musa utaikuta ya firauni, baada ya kukatisha mawasiliano nilishtukia Amina ameniekea mtutu wa bunduki kwenye kichwa kabla sijatamuka neno mlango ulisukumwa kwa kishindo na maaghulamu watatu wakaingia ndani. Sikuamini macho yangu, yaani Amina alikuwa jambazi, alitumwa kuchunguza siri zangu, akanitega na kuninasa barabara, kweli mapenzi upofu na si vyote ving’avyo ni dhahabu. Jambazi mmoja alinisukumia ngumi nzito kama mhalifu nikaanguka chini kama mlevi.
Kilichofuata sitambui kwani nilizirai. Nilijipata siku iliyofuata na ni nikapewa maelezo ya matukio yaliyonikumba.Amina alikuwa ameendea hati zangu na kunikwibia pesa yote niliyokuwa nimehifadhi banki pamoja na gari langu. Nilihisi ulimwengu umegeuka ghafla kuwa sumu iliyonikula na kuniacha ghofu la mtu. Niliona macho yakifumbika, vimulimuli vikitanda hatimaye giza nikawa nusu maiti. Dunia ni rangi rangile.

Use Facebook to Comment on this Post

Related Posts:

  • No Related Posts

About Richard Ngala

Check Also

Love can do it

Post Views = 2348 Before you begin to look for my hand, let me tell …

First dates

Post Views = 7427 I do realize that that my creative mojo isn’t back yet. …

2 comments

  1. Umejenga maudhui ya mapenzi thuluthi mbili na kuleta dhana ilobeba fungu hili kwa kiduju. Lapendeza fungu kulisoma.

Leave a Reply

Connect with:
Your email address will not be published. Required fields are marked *