Mlo si mlo

= 1255

Siku ya Jumapili huwa ni siku ya kujivinjari hapa na pale na marafiki, kuwa na matemebezi kiasi na kufurahia maisha. Na hii Jumapili nlikuwa nimeenda kumtembelea rafiki yangu mmoja jijini.

Kwa kawaida mazingira ya jiji huwa ni mazuri. Wikendi huwa tulivu na nyuso huwa zina furaha. Watu wanapumzika huku wakila raha pole pole bila fikira sumbua. Hamna kazi hivyo watu hawana haraka na maisha.

Watu hujitosa jijini kwa wingi, haswa jointi za nguvu na familizia zao. Ni siku ambayo kila mtu anaonyesha alicho nacho. Mavazi ya ulimbwende huvaliwa, sisemi yale ya klabu, bali yale mavazi ya kutangazia ulimwengu kwamba uko huru kuonyesha ulicho nacho.

Mimi kama kawaida, ije mvua ama jua, niko ndani ya kaptura, yaani suruari fupi ya vijana ambao hawajatahiri. Siku moja kijana moja alinambia ‘kaka mbona wavaa vinyasa? Vitu za watoto izo!’

Nami wajua kichwa ngumu nikamwambia, ‘hujalijua jiji kaka. Wavaao masuti na kujinyonga na tai kama waendao makaburini kufufua mfu hawana kakitu, sisi wenye vinyasa ndo twazungusha mji baba.’

Iyo ilikuwa siri ya ndani. Nairobi ina aina anuwai za watu. Kuna maskini, matajiri na pia wale wanaoitwa middle class. Apo mimi nikiwa kati ya wale wanaomiliki mji (those who run the city).

Rafiki yangu ywaita Hasara. Ni kijana mtulivu lakini mwenye hasira. Ni wale vijana bandia, hawana dira yoyote katika maisha, ila pesa wanayo. Mimi nami nmezoea kudoea kila mahali, toka chakula hadi binti wa wenyewe.

Nlipofika jijini ilikuwa saa tano asubuhi. Jua nalo lilikuwa lajisukuma kwa miguu mitatu, kwa nadhiri na umakini. Liling’aa kwa ujasiri na nyuso za watu zilikuwa zinawaka, na kwa wenye vipara ilikuwa kama mabati inayong’aa. Hivyo ikanibidi nitembee mkono moja ikia kwenye uso kujikinga toka ile miale mikali.

Nilipokuwa nimekwambia Hasara ni mang’aa mjanja, hivi ndivyo ilivyo. Kusema ukweli si wale watu mnaezapatana kwa urahisi mkianza kutafutana. Ikabidi tukutane pahali fulani palipojulikana ndo tusije tukapoteleana. Nami mwoga wa mwisho, cjatembea hili jiji la Nairobi nilijue vizuri.

Nlimkuta Hasara kahoteli fulani akiwa na marafiki wake wawiili. Kusema ukweli ckuwapenda. Mdomoni mwao mlikuwa vijiti vingi vikonde vikonde. Nlikuja kuelewa kwamba walikuwa wanachana miraa. Kando kando ya midomo yao mabaki ya iyo mizizi yalitapakaa, na walipoongea baadhi yazo yalikuja bila kusita hadi usoni.

Ilinibidi nimwite pembeni tubonge kidogo.

‘ karaha gani hii kaka? Wafanya nini na hao mikora?’ nikauliza nkiwa nmeudhika.

‘usijali brathee, hao mavijanaa wana fomu kuruka,’ akajibu uyo Hasara. Toka hapo nkamwona tu kama hasara. Nikashindwa ikawaje leo yeye, mtu ambaye namheshimu kanilet down hivyo.

Tulijikwamua mle pembeni tukarudi kule kwa wenzetu. Baada ya muda mazungumzo yakanoga. Bila kutarajia vinywaji vikaja kwa wingi.

Wajua mimi mtoto wa mama, nanywa maziwa na maji. Lakini hii siku matiti ya kunyonya hayakuwa karibu, ila michemko ya machupa. Nikajichukulia  Lemonedi na Fanta madiaba chupa tano. Zote hizi nikaziegesha mezani nkatafuta omo nkaosha tumbo.

Baada ya kukunywa hivyo vinywaji, tulichangamka. Marafiki zangu walikuwa wamekunywa chupa mbili mbili za Tusker. Wallahi nachukia harufu ya pombe.  Mimi kanywa mtungi mzima, tumbo ikanona kama mja mzito.

Wajinga ndo waliwao.

Tukatoka pale karibu saa nane kuelekea Zimmerman ambapo kulikuwa na sherehe ya Bathidei. Huko mimi mgeni. Kufika huko tukapata vyakula vimeandaliwa kwa wingi. Ubaya ni ule sikuwa na habari kwamba tungeenda mahali kula. Na Hasara hakunipasha habari yoyote kwamba huu ndo ulikuwa mpango. Ndo maana yeye na marafikize wakanywa chupa mbili mbili tu. Nkt!

Hapo ndipo nlisakamwa na hasira. Iweje nisiambiwe jambo la maana kama hili? Tukakaribishwa kwenda mezani kwa maakuli. Tukanawishwa mikono, mmoja baada ya mwingine. Kusema ukweli tumbo lilikuwa limejaa. Hakukuwa na hata tone moja la nafasi.

Nlipofika mezani mapocho pocho yalikuwa yananiangalia kwa uzuri. Ila tu hayakuelewa nlivyokuwa na nia ya kuyapakua yote kwa sufuria niyale hadi tone la mwisho la supu. Kulikuwa na kuku chemsha, chapati, na vitowea kadhaa.

Ndani ya moyo wangu nlivitamani hivyo vitowea mno. Kwa utulivu nkameza mate mazito. Na kwa woga nikwa na msuko suko wa kutokua na nafasi ya kuweka hayo mapocho pocho. Wakati huo nlisikia kutafuta kisu nkachinje hiyo tumbo,  nimwage hayo maji yote nipate nafasi ya kula. Lakini nafsi yangu ukaniambia la.

Basi akapita dada mmoja mrembo hapo. Nami nkamwuliza nipate wapi vile vyumba vya usafi.  Basi kwa ukarimu wake akaamua kunionyesha. Ckuwa naskia haja yoyote, kubwa ama ndogo, la hasha.

Nlipoviona nlikimbia ndani. Alafu nkafunga mlango. Kwa maana nlikuwa na ari kubwa ya kile chakula, nliingiza vidole mdomoni hadi kwa koo. Lazima ningetapika ile soda yote.

Basi katika harakati za kujaribu kutoa soda tumboni, jamaa mmoj akagonga mlango kwa kishindo. Hujui nilivyoshtuka. Hapo hapo nikasakwama (choked) koo na yale matapishi. Kwa dakika mbili hivi nkakohoa kama mbweha aliyesakamwa na mfupa wa ndovu kwenye koo.

Bahati haikuwa yangu.  Bila kujua lolote nkazirai, na kuanguka juu ya yale matapishi. Kwa siku moja nkawa nnahudumiwa hospitalini baada ya kulazwa.

Kitu cjui ni kwamba kama kuna mtu anajua ukweli huu. Ijapokuwa nlizimia na kutupa rada ya maisha, wallahi namiss ile chakula bado.

Kuwa na watu kama Hasara, ni hasara tupu. Tafhadhali tafuta marafiki watakaokunufaisha maishani. Toka hiyo siku rahgba ya mkanja nimeachia fisi. Ufisi ni gharama, na waweza kufa ukitaka mengi……nlilitambua jiji. Na toka iyo siku Jumapili haijakuwa siku nzuri kwangu tena, ni kama maradhi ya kuharisha.

Popote ulipo Hasara, wewe ni mtu bure sana. Ndio hivyo kulienda. Na uache ujinga.

-photo credit:imgkid.

Use Facebook to Comment on this Post

Related Posts:

  • No Related Posts

About Mzangila

Mentor, media consultant, photographer, editor, poet, writer, and counselor.

Check Also

Rise of the Phoenix

Post Views = 2331 People are resilient. I think we are designed that way. Its …

Of the house

Post Views = 3103 The thing about writing is that I don’t know whether it …

Leave a Reply

Connect with:
Your email address will not be published. Required fields are marked *