Dunia uwanja wa fujo I

Feel free to share 🙂
= 3169

Hakika dunia ni uwanja wa fujo lakini kila binadamu ameumbwa ili aufaidi kiasi cha awezavyo.
Basi nasadiki kuwa kila mtu ameumbwa duniani afanye fujo kisha ajiondokee.
Lakini je kuna uwezekano kuwa nimeshindwa kutimiza fujo yangu kabla nijiondokee?
Kamwe sitasahau fujo niliyo kumbana nayo katika ule msimu wa hangaiko la kutafuta pesa ya karo. Jalali hakika shukura zangu kwako uzipokee.
Leo hakika nina bahati ya aliyezaliwa ijumaa.Ali lilivyo jina lake siku hiyo alitekeleza fujo yake kikamilifu

Jioni hiyo nilipokea ujumbe uliokuwa wa siri kubwa kutoka kwa Ali naye alipogundua arafa yake kaituma kwenda pasipofaa alinipigia simu na kuniomba radhi niufute ule ujumbe ule. Kulingana na mafunzo ya wazee wangu basi nilimtendea matakwa yake . Aliposadiki kuwa ujumbe ule umefutwa aliniahidi zawadi ambayo alinuia niipate siku iliyofuata .
Usiku huo nilikosa lepe la usingizi .Niliwaza na kuwazua namna ningelipa karo iliyo kuwa imezalia alafu baadaye nijinunulie mawanda sita ya kisasa pamoja na njuti aina ya stiletto shoes.

Hakika dunia ni uwanja wa fujo. Siku ya siku hii hapa .”hello madam am I talking to Maria?”Baada ya salamu na kujuliana hali basi alinielekeza kuwa angenitumia hela inform of a cheque na hivyo basi niliweza kumpa nambari ya kitamburisho, nambari akaunti na majina yangu halisi .Akanielekeza nisubirie kidogo ilimradi awasiliane na wahuduma wa banki ya Mombasa ambayo wangefanya transactions. Baada ya risali mbili mhuduma wa banki alinialifu kuwa Mhisani wangu alisahau kulipia gharama ya muhuduma wa banki ya shilling elfu 6000. Katika hekaheka ya kukopa pesa bila mafanikio ndipo lilinijia wazo kuwa uendaikawa wahisani wangu hawa ni wa fujo.

??????????????????????????
??????????????????????????

Akilini niliamua kuwaelezea bayana kuwa kuzipata hizo hela limekuwa tatizo na hivyo kuwasihi waweze kunitoelea ile pesa ya transaction
Mary Hapa ndipo Wote walipopandwa na hasira nusura kupasuka Hakika dunia ni uwanja wa fujo siku hiyo niliweza kufasili dhana ya wale wakora.

***********************************************************

part II

Katika kutarihi uwanja wa fujo ,leo nimo mbioni kushiriki katika azmio la kutimiza fujo yake halafu kisha nijiondokee kwenda kwenye hatima yangu.Huenda lisiwe jambo la busara lakini nimenuia ujenzi kwenye uwanja huu wa fujo.

Iwapo hakika kupitishwa kwa mswada itakayonuia kukandamiza fikra za wanyonge basi huenda sina haki . Moyoni nina kichomi labda donda ndugu.

Hakika uneni uliotamkwa kwa mathumuni ya kuleta uelewa umewasha mwako wa fujo. Lau ningejua katu singetoa mawazo yangu .Heri hata yangenila yakipenda yanibakishe.

Hamkani si shwari tena . Kumbe kunena haki no kama kuwasha mwako wa fujo nyoyoni.
Hakika maji nilishaweka na sina budi kuyaogea. “Siwezi kuwa natawaliwa kama mfungwa. Hakika nahitaji uhuru si wa mavazi,mila,uraibu,elimu na mtagusano wa hisia zangu basi kuwa na vizuizi.Ifahamike bayana kuwa kila mtu ameumbwa duniani afanye fujo yake halafu kisha ajiondokee.
************************************************************

Leo hakika nina nuia kuvumbua fujo yangu kabla nijiondokee. Azimio langu ni kuzua amani; fujo ya amani. Kuishi kama mbingu na ardhi basi kutagusana si haki. Aguta ukatili wako umenizidi si tena sehemu mtimani kuhifadhi dharau na dhuluma zako. Mara ngapi umesababisha machungu moyoni ? Lau ungeelewa hakika sina mengi ya kunena inshalla umenipa funzo basi sina radhi ila kulienzi.
Hakika sithamini maongezi yangu nawe. Umefika wakati ambapo kujinyamazia ndiyo dawa ya donda langu.
Sukusadiki jioni hiyo niliweza kufasiliwa namna ambavyo kisomo changu kimekufurisha na kukivimbisha na madharau.Msaada wetu kwako uwe ni kikomo tangu leo.

Kumbe kweli kila mtu anazo njia zake za kupokea, kufasili na kuwasilisha maoni yake. Sadiki sinuii kuharibu mwana, nanuia ujenzi.lakini je utajengaje na kila mtu yumo katika harakati yake ya kutimiza fujo yake halafu kisha ajiondokee? Huenda ikawa nimeshindwa kutimiza fujo yangu ya kuleta amani ila tu nimezua wingu la machozi machoni pangu sina budi nimombioni kutimiza fujo yangu kabla nijiondokee . Inshalla

BY MARY OYUGI:0722170603

Use Facebook to Comment on this Post

Related Posts:

  • No Related Posts

About Mzangila

Mentor, media consultant, photographer, editor, poet, writer, and counselor.

Check Also

Old times in a new era

Post Views = 2686 I joined my old man in the front porch. I pulled …

Why your son will never play in the EPL

Post Views = 2473The world cup starts in less than three days and football is …

2
Leave a Reply

Connect with:avatar
2 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
2 Comment authors
Richard MuriguDyson Recent comment authors
  Subscribe  
newest oldest most voted
Notify of
Dyson
Guest

Katika riwaya hii Dunia uwanja wa fujo mwandishi amejitahidi kwa kiasi kikubwa kuonyesha maudhi mbalimbali katika kazi yake kupitia vipengel;e mba 1000 limbali kama vile Dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo itikadi hii yote ni kwa lengo kuu la la kuelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali yanayotukia katika jamii hiyo.

Richard Murigu
Guest

Riway nzuri kabisa,yafaa kusomwa shuleni miaka ijayo